GET /api/v0.1/hansard/entries/1222959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222959,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222959/?format=api",
    "text_counter": 58,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Saa hii tunachimba madini kule Kwale. Ni madini ambayo kitaalamu inasemekana yanapatikana hapa Kenya kwa wingi. Ni madini yaliyo na thamani. La kushangaza ni kwamba madini hayo yanachimbwa na kuhesabiwa kama mchanga, yanawekwa kwa macontainer, yanapelekwa bandarini na kusafirishwa nje. Sioni ni kitu gani ambacho kingehitajika zaidi kuhakikisha kwamba madini hayo yanawekewa kiwanda. Sisi hatuna matumizi ya haya madini yanayochimbwa. Moja kwa moja yanatumika katika nchi za ng’ambo. Kwa hivyo ni wazi tuyapeleke kule. Lakini, kwa nini tunapeleka madini ama rasilimali yetu ikiwa bado haijatengenezwa? Najua Serikali itatilia maanani Hoja hii ili kuhakikisha kwamba raslimali zetu, ambazo Mwenyezi Mungu ametujalia, zinatengenezewa viwanda humu nchini ili ziboreshwe na tupate ajira na thamani zaidi ya ile ambayo inapatikana hivi sasa. Kuna suala ambalo linatumaisha. Endapo tutaleta thamani hizi katika nchi yetu, ni lazima kuwe na vigezo ambavyo vitasaidia hili kufanyika. Tunajiuliza ni kwa nini wengi waliokuwa na viwanda hapa, mbali na kuwa hawakuwa hata katika hizo sehemu ambazo tunatarajia ziweze kupewa mkazo wa kutengenezwa kwa minajili ya kupeleka nje, wanahama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}