GET /api/v0.1/hansard/entries/1222960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222960,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222960/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "kutoka nchi hii na kufikiria kuekeza sehemu nyingine. Hii inatokana na ile miundo-misingi ambayo tuko nayo. Kwamba, wakati wowote ambapo tunataka kuweka sehemu kama hizi, basi wale mabwenyenye ama wakora hujiingiza pale. Ni kwa sababu wao hujua mapema kwamba Serikali inanuia kufanya sehemu fulani eneo la kuzalisha bidhaa za kupeleka soko la nje. Basi mabwenyenye huingia katika sehemu hiyo na kunyakua ardhi. Hatimaye inakuwa vigumu kwa Serikali kupata ardhi kwa urahisi ili kutengeneza viwanda. Endapo nafasi hii inapatikana, kuna suala zima la kawi ya stima. Tukizungumzia mambo ya kutengeneza vitu, moja kwa moja ni lazima stima ama mafuta yatatumika pale. Tunajuwa stima ama mafuta yako bei juu. Wakati tunazungumzia suala hili na kuona kwamba tungetaka tuwe na viwanda hivi, inabidi serikali iangalie suala la ni vipi stima ama mafuta yatakuwa bei ambayo mwekezaji ataweza kumudu ili atakapotengeneza hizi bidhaa, zitakuwa imara na zenya bei ambayo ni nafuu kule nje. Hivi sasa, utakuta kwamba kwa sababu ya gharama za stima na mafuta, bei ya bidhaa inakuwa juu zaidi. Hilo linafanya kuuza bidhaa hizo nje mwa chi inakuwa vigumu. Nina imani Serikali iliopo sasa inayo miundo-misingi na mikakati ya kuona kwamba bei ya stima inashuka. Naamini kwamba Wabunge kwenye upande wa Serikali watasaidia kupitisha Hoja hii ili isibaki kuzungumziwa tu bali iweze kutekelezwa ili watu wetu wapate ajira. Tukizungumzia suala la viwanda kwa minajili ya kupeleka bidhaa katika nchi za ng’ambo, tujue kwamba kuna vijana wengi ambao wana maono. Wamevumbua vitu tofauti tofauti. Nakumbuka kinyume kulikuwa na taratibu za kuona kwamba wale wanaoweza kuvumbua wanawekwa mahali fulani ili wajiendeleze, kupata mawazo zaidi na kusaidika. Lakini, mbali na hapo, hakujakuwa na hatua zozote za kuona ni vipi walio na akili na uwezo wa kuvumbua vitu wanasaidiwa na Serikali, ama ni mikakati gani Serikali inaweza kuweka kuwashikanisha na watu binafsi ili waweze kutekeleza na kuunda bidhaa hizo kwa wingi ili waweze kuziuza katika masoko ya ughaibuni. Hivi sasa tunanunua simu za mkononi. Nina amini kwamba hili ni jambo ambalo lilianzishwa na mtu mmoja ama watu wachache lakini serikali husika kule ughaibuni ziliwasaidia – ziliwaweka mahali, zikawapatia hifadhi na kuwapatia usaidizi waliohitaji kuona kwamba wanazitengeneza. Hatimaye kila mtu ananunua simu ya mkononi hivi saa. Biashara hiyo, moja kwa moja, inanufaisha kule zinakotengenezwa. Hapa kwetu kuna vijana ambao wamevumbua ni vipi wanaweza kuendesha gari wakitumia maji na ni vipi wanaweza kutoa mwangaza wakitumia moshi, lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote ambazo Serikali imechukua. Hilo limeleta tatizo kubwa la ajira. Raslimali tunazo na akili tunazo, lakini hatujakuwa na msimamo na miundo-mbinu ambayo inaweza kutusaidia. Kwa hivyo, hii Hoja ni ya kuzingatiwa. Ni ombi langu kwamba isibakie Hoja lakini iweze kuambatanishwa na sheria. Kisha tutaona kweli hizi sehemu za kuzalisha na kupeleka nje zinadumishwa. Kama mwenzangu alivyonena, tuna tatizo kubwa la sarafu za kigeni hivi sasa. Hii ni kwa sababu hatuna kitu chochote cha maana ambacho tunauza nchi za nje. Wakati huna kitu chochote unachouza katika nchi za nje na ni wewe tu unanunua kutoka nchi za nje, inamaanisha kidogo ulicho nacho katika sarafu za kigeni ndicho kinatumika. Hali hii ikiendelea, itafika wakati Kenya nzima kwa jumla hatutaweza kujisimamia hata kwa bidhaa tunazohitaji kila siku. Ni kwa sababu hatuna chochote ambacho tunatengeneza kutuma nje ili kituletee sarafu za kigeni. Nakushukuru. Naunga mkono Hoja hii mia fil mia."
}