GET /api/v0.1/hansard/entries/1222976/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222976,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222976/?format=api",
    "text_counter": 75,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohammed Ali",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, ninaomba kutoa Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukifahamu kuwa, familia ndiyo kiungo cha msingi cha jamii na kutambua kwamba utamaduni wa Kiafrika unathamini sana asasi ya ndoa ambayo inahakikisha kuendelea kwa binadamu kupitia uzazi; tukizingatia ukweli kwamba, Ibara ya 45(2) ya Katiba inaeleza kuwa kila mtu mzima ana haki ya kufunga ndoa na mtu wa jinsia tofauti kwa msingi wa hiari baina ya wahusika; tukitambua pia kwamba Kifungu cha 162 cha Kanuni ya Adhabu kinamutia hatiani yeyote ambaye anashiriki tendo la ngono lisilo la kawaida na mtu yeyote kinyume na utaratibu wa asili; tukizingatia kuwa mahusiano na ndoa za jinsia moja na ngono inayotokana na mahusiano haya ni kinyume na utaratibu wa asili; tukisikitika kwamba kumekuwa na ongezeko la mahusiano ya jinsia moja nchini Kenya kutokana na usambazaji wa vitabu na machapisho yanazokuza upotovu huo; tukitambua kwamba uchapishaji na usambazaji wa nyenzo zinazohusu mahusiano ya jinsia moja katika machapisho na vyombo vya habari una athari kali kwa maadili ya jamii kuhusu mweleko wa kijinsia; tukimaizi kwamba, kuna haja ya kutekeleza sheria ili kulinda na kuhifadhi maadili ya mahusiano ya jinsia tofauti katika taifa; tukifahamu kwamba hakuna uwezekano wa kuzaa kutokana na mahusiano ya ndoa za jinsia moja; tukihofia kwamba kuongezeka kwa mahusiano na ndoa za jinsia moja kunaitia jamii ya wanadamu nchini katika hatari ya kutoweka; Bunge hili, hivyo basi, linaazimia kwamba Serikali ipige marufuku mara moja uzungumziaji, uchapishaji na usambazaji wa taarifa zinazokuza mahusiano ya jinsia moja nchini na kuweka mikakati ya kudhibiti maudhui hayo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}