GET /api/v0.1/hansard/entries/1222979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1222979,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222979/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohammed Ali",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, ninawasilisha Hoja hii kirasmi. Shukrani sana. Kama nilivyotangulia kusema Mhe. Spika wa Muda, ni kwamba kumekuwa na taarifa zikichapishwa kuhusu tabia potovu inayoenda kinyume na maumbile nchini Kenya. Tabia hiyo imeanza kukita mizizi. Sisi kama viongozi ni jukumu letu kusimama na kupinga maovu ambayo hayakubaliki katika dini zetu, utamaduni wetu, na asili yetu. Jambo hili geni linaletwa na watu kutoka mataifa ya nje ili kuliharibu Bara la Afrika. Hapa Kenya mjadala huu umekuwepo kwa muda sasa. Vyombo vya habari vimekuwa vikizungumzia, kwa kimombo, Lesbian, Gay, Bisexual, Transgender, Queer, Intersex andAsexual (LGBTQIA). Lakini ninataka kusema kwa ufupi kwa lugha ya taifa: tunapinga watu wanaoenda kinyume na maumbile, yaani mashoga na wasagaji. Mashoga ni wale wanajamiana, wanaume kwa wanaume; na wasagaji ni wale wanajamiana, wanawake kwa wanawake almaarufu lesbians . Mhe. Spika wa Muda utamaduni wetu Waafrika haukubali hii tabia ambayo hata wanyama hayawani hawafanyi. Mnyama mwenye sura mbovu zaidi, fisi, hashiriki tabia hii ambayo binadamu wengine leo hii wanafanya. Wanyama ambao tunawaona kama hayawani hawafanyi yale ambayo binadamu wengine wameanza kufanya. Hii ni kwa sababu ya utumwa unaotokana na kuja kwao humu nchini kisha wakaanza kudharau na kutesa Waafrika. Walianza kufunza watu tabia za jamii zao na kuingiza fikira zao potovu ndani ya Mwafrika. Hivi leo, kuna Waafrika ambao hawapendi rangi ya ngozi yao. Yaani kuna Mwafrika hajipendi. Kuna wale ambao wanatumia dawa kuongeza maungo mbalimbali mwilini; wengine wanatumia dawa za kuwageuza wawe weupe; na wengine wanakaanga nywele zao ili zikaribie zile za Wazungu. Lakini ni Wazungu ndio wanaharibu dunia kwa kuleta tabia ambazo hata mwenyezi Mungu hataki. Wacha nirudi katika dini maana wanasema ni world order mpya wanayotaka kuleta. Wanataka kuangamiza ulimwengu. Hawa ni watu wasioamini kuwa Mwenyezi Mungu yuko. Wao wanaamini sayansi. Wanaamini kwamba jinsi dunia ilivyo na jinsi mambo yanavyotokea ni kwa sababu ya sayansi wala siyo Mwenyezi Mungu. Nitaanza Hoja hii yangu kwa kunukuu vitabu vitakatifu. Nitaanza na Quran ili tuweze kusawazisha haya mambo. Nimeona jinsi wanavyokuja, tusipokuwa makini kama viongozi, nchi itaharibika na uzazi utapungua. Kenya itakosa watoto, nguvu kazi, na hatimaye italaaniwa. Mungu atatuadhibu kwa sababu ya kwenda kinyume na maumbile."
}