GET /api/v0.1/hansard/entries/1222984/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222984,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222984/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohammed Ali",
"speaker": null,
"content": "Hatutakubali nchi hii ipotozwe na Wazungu walioleta dhuluma, na wanaotembea katika dunia kuleta dhuluma. Wamemaliza shughuli zao Uarabuni sasa wanaingia Bara la Afrika kulimaliza. Wanakuja na kisingizio cha haki za binadamu. Hakuna haki ya ushoga wa mwanaume kwa mwanaume kupandana. Hakuna haki ya mwanamke na mwanamke kupandana. Hizo si haki za kibinadamu; hizo ni haki za kishetani! Soma vitabu vitakatifu. Inasemekana kulikuwa na Adamu na Hawa ( Adam and Eve ). Hakuna mahali pameandikwa kulikuwa na Adamu na Steve. Kuna mahali katika Bibilia pameandikwa, “Adam and Steve”? Hata shetani, ambaye anamwogopa Mwenyezi Mungu, alipoanza kuleta majaribu, alimwendea Eve; hakumwendea Adamu. Shetani mwenyewe anajua hilo halikubaliki, lakini sisi binadamu tunataka kuanza kujifanya sisi tunaweza kupinga dini ya Mwenyezi Mungu. Sisi tunaweza kuketi pamoja tutunge sheria ya kupinga jambo. Lakini ifahamike wazi kwa wale ambao hawajui: huwezi kubadilisha hata herufi moja katika Bibilia wala Quran. Katika Katiba unaweza kubadilisha jambo, lakini katika neno la Mungu huwezi kubadilisha herufi wala sentensi kwa maana hayo ni maandiko yake Mwenyezi Mungu. Leo, vyombo vya habari vinasaidia kueneza uchafu huu. Katika madarasa shuleni watoto wetu wanafunzwa mambo haya. Vitabu vinachapishwa. Angalieni nchi jirani ya Tanzania: Waziri mhusika wa elimu amepiga marufuku vitabu mbalimbali ambavyo vinatumiwa nchini humo kuleta uchafu. Wamepiga marufuku vitabu hivyo. Sisi hapa Kenya ni kusema tu eti mambo hayo hayatuhusu. Wakati mwingine tunasema eti ni demokrasia! Demokrasia gani hiyo? Demokrasia ya kijambazi! Katika silabasi za elimu, watoto wetu wanafunzwa eti familia inaweza kuwa na mama wawili na mtoto ama baba wawili na mtoto. Familia itakuwaje na baba wawili ama mama wawili ikiwa huo si ushoga ama usagaji? Wanataka kuchafua watoto wetu ili kizazi chetu kiangamie. Mhe. Spika wa muda, watu wanaogopa kulizungumzia suala hili kwa sababu wengi wao, hususan viongozi, wanajua wakimpinga Mzungu na yale yote anasema, basi Mzungu atawanyima visa . Leo nataka niwe mfano bora ndiyo ninyimwe visa. Mimi, Mohamed Ali, nasimama hapa kusema kuwa hatutaruhusu mashoga na wasagaji katika taifa hili. Sisi hatuko duniani kutafuta visa . Hatuko duniani kutafuta visa ya kuenda Marekani ama kuenda Ulaya ama kuenda mataifa mengine. Tuko hapa duniani kupata visa ya kutafuta ufalme wa mbinguni."
}