GET /api/v0.1/hansard/entries/1222994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222994/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohammed Ali",
"speaker": null,
"content": "Wazungu wanakuja humu nchini na mambo. Leo wanajiita ‘Viranja wa dunia.’ Jana nimeona Balozi wa Marekani ameweka katika mtandao wa Twitter kuwa amekuwa na kikao na hawa watu ambao wanajiita (LGBTQIA ). Aliwahakikishia kuwa haki zao zitalindwa. Haki za kila Mkenya zitalindwa, lakini si haki za kishoga na uchafu. Nenda katika mataifa yao na utagundua kwamba wao ni watu wa sayansi. Kwao, Mungu hayuko. Wanasema hawaamini Mungu. Wameleta uchafu duniani. Kwao, hata ni demokrasia binadamu kulala na mbwa! Wamefanya mambo ya ajabu ajabu duniani. Kwao, wanaogopa kuzaa kwa sababu hawajaekeza katika familia. Wanadai kwamba ukizaa hutakuwa na mtu wa kumwachia mtoto mchanga. Utaachia mtoto wako nani? Ndiyo maana unaona katika mataifa hayo watu wanaogopa kuzaa. Wakija katika Bara la Afrika wanaona tofauti kubwa: wanaona dini na utamaduni wetu. Wanaelezewa asili yetu, na wanaona ukuruba wetu. Mungu amefanya Bara la Afrika tajiri lakini umasikini wa fikira na uongozi umejazwa hapa kwa sababu hatujipendi. Hatukubali mambo yetu kama Waafrika ilhali tunakubali mambo ya wazungu. Akija Mzungu hapa na ashute, mtasema ni marashi!"
}