GET /api/v0.1/hansard/entries/1222996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1222996,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222996/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohammed Ali",
"speaker": null,
"content": "Mwafrika akifanya vile vile, mtasema ni uchafu! Hivyo ndivyo tumejidhalilisha. Hivyo ndivyo tumejichukia na ndiyo maana sasa wameanza kufikia watoto wetu. Ushoga na usagaji unazungumziwa kila mahali. Serikali ni lazima iwe kali na itoe adhabu kali. Katiba ya nchi ya Kenya imekataa tabia hizo. Hatukubali! Katiba imekataa. Bibilia na Quran zimekataa. Dini zote zimekataa. Ule uamuzi na maneno yaliyotajwa na Mahakama ya Upeo ni makosa; waliteleza. Lakini warekebishe maamuzi yao ili Wakenya wawasamehe. Binadamu si kamilifu maana yeye huteleza. Mahakama ya Upeo kusema kuwa hapa Kenya tumewapatia nafasi hao wanaokwenda kinyume na maumbile eti waunde Non-GovernmentalOrganisation ( NGO) ndiposa wajulikane ni wangapi na wasaidike, hilo hatukubaliani nalo. Hatuwezi kuwa na mashirika ya mashoga nchini Kenya wala hatuwezi kuwa na mashirika ya wasagaji nchini Kenya. Mashirika yakutusaidia ni yale ambayo yanamwogopa Mwenyezi Mungu na kuheshimu Katiba ya Kenya. Sharti yawe ni mashirika ambayo lengo kuu ni kuliinua taifa hili wala siyo kulipooza. Wale wote wanaofanya tabia hii, labda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}