GET /api/v0.1/hansard/entries/1223006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223006,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223006/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Kiwango cha pili ni baada ya kubwaga viatu, watu wanaanza kutamauka ambayo inaitwa ‘outlet’ . Watu wanashangaa ni vipi huyu mtu analeta jambo hili la ajabu. Ni vipi mtu anazungumzia suala kama hili ambalo haliwezekani? Huwa ni katika zile taratibu za kuona ni wakati gani jambo hili litakubalika. Kiwango cha tatu ni hiki ambacho tuko sasa. Tumeanza kulizungumzia jambo hili. Hulipendi, linashangaza, na ni la kipuuzi lakini inabidi tuanze kulizungumzia kama tunavyolizungumzia sasa. Nampongeza sana Mhe. Mohamed Ali kwa kuleta Hoja hii na kuhakikisha tunakomea katika nukta hii ya tatu ya kuzungumzia jambo hili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}