GET /api/v0.1/hansard/entries/1223007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223007,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223007/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Baadaye tutaingia ile hatua ya nne ambayo watu huanza kusema, ‘Shauri yake. Kama mtu ni shoga, ni ushoga wake.’ Kuna wengine ambao husema ushoga wa siku moja si ushoga. Ukishaanza tabia hii, ni kama vile mchovya asali ambaye hachovyi mara moja. Kumbuka kuna shinikizo kutoka nchi za kigeni ambazo zimeanza kuleta misaada na kuwapatia watu pesa kibinafsi siyo kwamba wasaidie jamii, lakini waendeleze tabia hizi. Nasikitika. Tangu jambo hili liibuke, inasemekana, samahani, kwamba kuna wenzetu katika hili Bunge ambao wamepatiwa fedha ili waweze kushinikiza wenzao washirikiane na mataifa ya kigeni kuendeleza na kupeana kipaumbele ushoga, usagaji na mambo mengineyo machafu. Ifikiapo hapo, nimesema samahani."
}