GET /api/v0.1/hansard/entries/1223014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223014,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223014/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Nilikuwa nimefikia kiwango cha nne ambacho ni watu kuanza kukubali. Nimesema kuna nukta sita katika masuala kama haya. Kiwango cha tano ni kile ambacho kitendo kinakubalika yaani mtu akifanya basi ni shauri yake. Tatizo lipo katika kiwango cha sita ambacho watu huanza kushabikia: ukiwa shoga au msagaji basi wewe umeendelea zaidi. Wewe sio mshamba na unajua ulimwengu jinsi ulivyo. Kiwango ambacho tumefika cha tatu cha kulizungumzia suala hili, naomba tukomee hapo. Ni jukumu la Serikali na viongozi kupeana mwelekeo na kuhimiza maadili mema. Ni jukumu la Serikali kuchukua msimamo wazi wazi, kinagaubaga, peupe, na mchana kwamba katika nchi na jamii hii hatuwezi kuruhusu, kukubali, kuendeleza, na kushabikia machafu kama haya. Wale ambao pengine wana fikira kama hizo na wanajaribu kushawishi wenzao wajiulize: je, kama wazazi wao wangekuwa wa jinsia moja, yaani baba wawili ama mama wawili, wangezaliwa? Watakuambia kwamba sayansi imeendelea siku hizi. Eti wazazi wanaweza kuwa jinsia moja halafu watumie sayansi kupata mtoto. Hakika haya ni mawazo ya kishetani ambayo hatuwezi kuyakubali."
}