GET /api/v0.1/hansard/entries/1223017/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223017,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223017/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Ikiwa utaogopa kuzaa mtoto kwa sababu hali ya maisha ni ngumu, Sheikh Mohamed Ali ametuambia kuna aya inayosema kwamba riziki inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Unaweza kuwa na mtoto mmoja na bado ukose kumlea vizuri; unaweza kuwa na watoto wengi na uweze kuwalea vizuri. Haya masuala ambayo yanafanya tunajipatia shida mpaka tumefika kiwango cha kuogopa kuishi vile Mwenyezi Mungu anavyotaka, yanahitaji kukemewa. Ni jukumu la Serikali kutoka peupe kupinga na kuilinda jamii yetu ili iwe na msingi mzuri kama ilivyo desturi yetu na vile Mwenyezi Mungu anavyotaka. Naunga mkono Hoja. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}