GET /api/v0.1/hansard/entries/1223023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223023,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223023/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": " Shukrani Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpongeza Mhe. Mohammed Ali ambaye amewasilisha Hoja hii. Baada ya yeye na mwenzake kuiafiki Hoja kwa lugha sanifu ya Kiswahili, sina budi bali kujikakamua kuzungumza Kiswahili changu chote cha bara, mradi tu niwasilishe yale ninayo. Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Masuala ambayo tunajadili leo katika Ukumbi huu tungeyajadili miaka iliyopita, ingekuwa ni mwiko. Hii ni maana kuzungumzia hayo masuala kwa mila na tamadhuni zetu, haingekuwa jambo la kawaida. Lakini, imebidi tuyajadili maana ni mambo ambayo yamekuwa yakisambaa. Kwa lugha ya kisasa itasemwa kwamba yamesambaa ‘chini ya maji’. Leo hii yamejitokeza wazi na kwa njia ya kutatanisha sana: kwamba, Mahakama ya Upeo imetoa uamuzi kuwa yale makundi ya mashoga na wasagaji yatambulike nchini Kenya. Uamuzi huo ulinistua sana maana ukisoma Katiba yetu, Ibara 45(1)(2) hadi (3) inazungumzia kwa kipana na kirefu maana ya familia, na aina gani ya familia zinatambulika. Ningependa kuwarai Wabunge wenzangu katika Jumba Hili kwamba, tunapojadili Hoja hii lazima turejelee wale Majaji ambao walitoa haya matamshi. Suala tunalojiuliza ni: Majaji hao walizungumza wakiongozwa na nini haswa mpaka wakahalalisha jambo ambalo limepigwa marufuku na Katiba ya Kenya? Ndiyo maana Bunge linafaa kuwapiga msasa wale wanaoteuliwa kuwa Majaji, Majaji Wakuu, ama wanaoketi katika tume tofauti. Hivyo, tutajua maadili yao ni yapi. Tusipokuwa waangalifu, labda, kuna mashoga na wasagaji kwenye Mahakam ya Upeo ndiposa wakatoa maamuzi wa kutatanisha kama tulivyoshuhudia. Kenya ni nchi inayoongozwa na Katiba. Pia iko na msingi wa kidini haswa Ukristu, Uiislamu na Hindi. Dini hizi zote zimepiga marufuku tabia ya ushoga na usagaji. Ni ajabu sana kuwa Mwenyezi Mungu aliumba binadamu kwa njia ambayo yeye pekee ilimpendeza; akaweka tundu kadhaa na tofauti katika sehemu za mwili. Kuna tundu katika masikio na kazi yake ni kusikia; kuna tundu katika mdomo na kazi yake ni kuingiza lishe The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}