GET /api/v0.1/hansard/entries/1223024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223024/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "mwilini; na tundu lingine lipo la kuondoa uchafu mwilini ambalo wengine wanataka kugeuza liwe la kazi nyingine. Hayo, ni makubwa sana. Lakini cha kutisha mno ni kwamba wakoloni walikuja kwetu na wakatuonyesha kuwa kila kitu ambacho kinaambatana na mila zetu ni kibaya. Pia, kila kitu cheusi ni kibaya. Wametengeneza na kutuletea filamu zao zinazomwonyesha shetani kuwa na rangi nyeusi. Labda shetani alikuwa mweupe pe pe pe, hatujui! Tulitiwa kasumba ya kuchukia kila kitu chetu ambacho ni kizuri na kununua yale ambayo ni mabaya. Sasa, wamechukua hatua nyingine kwamba sharti ufanye hili ama lile ndiyo watoe misaada fulani. Mimi nataka kuwaambia Wakenya na Wabunge wenzangu, afadhali tuwe maskini jeuri na hata tufe njaa maanake, Mwenyezi Mungu hakutuumba tufe njaa. Tunaeza tukafa na shida zingine lakini tusije tukaambiwa hapa na beberu kwamba tupitishe Mswada wa kukubali ushoga na usagaji ndiyo watupe misaada. Afadali misaada yao ikae maana, mimi ninavyoona, wanasema malipo ya kila kitu ni hapa duniani. Wale wabeberu walitutawala miaka ya awali na ukienda kwao leo hii, hali si hali tena. Hawazai na mke na mume wakioana, hawataki watoto. Wao hubeba vijipaka na vijibwa katika magari yao. Wengine wanaoana mwanamke na mwanamke ama mwanaume kwa mwingine. Mimi ninaona kwamba, labda, ni mpango wa Mwenyezi Mungu kuwa hivi karibuni, atatupatia sisi Waafrika, urithi wa hii dunia nzima. Kama hawa watu hawatazaa, sisi tutawarithi tu. Tunanaomba Mungu iwe ni kwa miaka ambayo tutakuwa hai. Kwa hivyo, ninapounga Hoja hii ambayo imewasilishwa na Mhe. Mohamed Ali mkono, ningependa kusema kuwa tunahitajika kupiga marufuku chochote kile ambacho kitaonekana kushabikia tabia hii potovu. Hii ni tabia ambayo hata Mwenyezi Mungu hakubaliani nayo. Nami nikiangalia kwa utaratibu, naona hata shetani mwenyewe hawezi kukubaliana na tabia hiyo. Kwa hivyo, naomba Bunge hili, kupitia kwa Wabunge wenzangu, tufanye vyovyote vile, kadri ya uwezo wetu, kuokoa vizazi vyetu. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu alituteua na kutupa sauti ya kuzungumza kwa niaba ya wale watu wetu ambao hawawezi kufika katika Ukumbi huu. Hapo tutaweza kuokoa vizazi vyetu, watoto wetu, na kulinda familia. Katika Ibara ya 45 tumeambiwa kuwa Katiba ya Kenya inatambua na kulinda familia. Kwa hivyo, ni sharti tushabikie ulindaji wa familia kama msingi wa jamii. Mhe. Spika wa Muda, naomba kumalizia hapo. Naunga mkono Hoja iliyowasilishwa na Mhe. Mohamed Ali."
}