GET /api/v0.1/hansard/entries/1223025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223025,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223025/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Martha Wangari",
"speaker_title": "Spika wa Muda",
"speaker": {
"id": 13123,
"legal_name": "Martha Wangari",
"slug": "martha-wangari"
},
"content": " Asante, Mhe. Sarah Korere kutoka Laikipia Kaskazini. Tunapoendelea, ningependa kuwakumbusha kwamba tunatawaliwa na sheria zetu – Kanuni za Kudumu. Hata ingawa haukubaliani na maneno yaliyosemwa na mtu mwingine: “87 (1) Hairuhusiwi kudhalilisha mwenendo binafsi wa Rais, Spika, Jaji ama mtu yeyote anayetekeleza majukumu ya kimahakama…” Ni vyema pia tutilie hayo maanani katika michango yetu na tuweze kufuata sheria vilivyo. Nataka nimpe sasa wakati huu, Mbunge wa Kinango, Mhe. Gonzi Rai."
}