GET /api/v0.1/hansard/entries/1223026/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223026,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223026/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika Wa Muda, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kunipata nafasi hii. Tunasema kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na ndogo ndogo, ametupa uwezo wa kuweza kuingia katika Bunge hili ili kujadili maovu na mazuri. Hivi ni kuhakikisha kwamba tunaweka wananchi wetu pahali panapostahili. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu na pia Mbunge wa Nyali kwa sababu ya kuileta Hoja hii kwa wakati unaofaa. Mwanadamu anapoishi katika ulimwengu anakumbana na mambo mengi. Labda, kutokana na Hoja hii, baadhi yetu tutaanza kufungua masikio na kujua kwamba kwa hakika tuliyapenda ya Mzungu na mmishonari lakini hivi sasa yanatupotosha. Umaskini sio kilema. Udhaifu na unyonge usiwe sababu yetu kufikishwa mahali ambapo tumefikishwa sasa hivi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}