GET /api/v0.1/hansard/entries/1223027/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223027,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223027/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Ni jambo la kuhuzunisha sana. Mmishonari na Mzungu walipoingia hapa, kwanza alianza kudharau mavazi yetu. Akaanza kutuvisha makoti ilhali sisi tulikuwa tunavaa ngozi. Akatuvisha makoti na akasema kwamba haya ndiyo yatakuwa mavazi rasmi. Wakati wa jua, nchi kama hii yenye joto la karibu nyuzi 40 na bado unalazimishwa kuvaa koti. Huna la kufanya kwa maana umeambiwa hayo ndiyo mavazi rasmi. Akaja tena akatuletea tai. Akasema tufunge hata wakati ambapo kuna joto. Tunaambiwa tufunge tai ilhali ni mavazi ya mtu ambaye ametoka Canada mahali ambapo kuna baridi. Tuliyakubali haya yote kwa sababu hatukuwa na budi. Wakati umefika ambapo ni lazima watu waanze kuambiana ukweli. Tumeyavumilia, tumeambiwa, na tumeonyeshwa mengi. Lakini kama tulivyosema hapo awali, umefika wakati wa kujisimamia. Hii ni kwa sababu tunachokitambua sisi katika ulimwengu, iwe ni Mzungu au Mwafrika, ni kitabu cha Zaburi, Torati, Injili na Quran . Hayo mengine tunayoyafanya kama wanadamu, yameanza kutuletea madhara. Kuna wakati utafika tuambiwe, ‘Kama hamtakubali mambo haya, hamtapewa visa tena.’ Sasa, unapewa visa kwa sababu umekubali kuwa shoga au msagaji ili ukifika kule uwe chakula cha binadamu wengine? Tuliambiwa kwamba tuwe na uvumilivu. Walipoanza kutubadilisha kikweli, walifika mahali wakatuletea nywele bandia na hivi sasa zimebadilisha sura za wake zetu. Tumezikubali na tunajua kwamba kila mwanadamu ana nywele na huruhusiwi kuzikwa na hizo nywele bandia. Mhe. Spika wa Muda, tutakanywa namna gani? Tulipewa siku saba; Ijumaa, Jumamosi na Jumapili twende tukaombe. Hayajatutosha! Kutakuja kuwa na siku ya usagaji duniani. Hayo pia yanakuja. Na ni lazima tuyakubali. Haya siyaoni katika kitabu chochote cha Mwenyezi Mungu. Lakini sisi twayatukuza kwa sababu ya kuhitaji misaada. Miaka 50 iliyopita, nakumbuka dhahiri katika ujana wangu, hakuna wakati ambapo sisi tuliomba Serikali itusaidie chakula. Ni kwa sababu nchi ilikuwa ina rotuba na mvua ilikuwa inanyesha kwa misimu yake. Yawapi hivi sasa? Ardhi imekataa. Kumbukumbu na historia zinatuambia hata wana wa Israeli walipokuwa barabarani kuelekea Canaan, wakitoka kule kwa Firauni, walifanya ubishi, ardhi ikafungwa ikawa haitoi chakula na anga haitoi mvua. Shida ikapatikana papo hapo. Ninafikiria ilifika wakati Mwenyezi Mungu alipoombwa, aliwajibu kwamba, ‘Katikati yenu kuna mnafiki.’ Je, nani ni mchawi katika matatizo haya yote? Tuiulize Serikali. Ndiyo maana tunaiambia kuwa jambo hili tunalizungumza hapa Bungeni na tunachokiomba ni kwamba itakapokuwa Wabunge hawa wamekubali kulipitisha, wajue kwamba kuna umuhimu wake. Walipokuja hapa, walituambia tupange uzazi na walipoona tunakataa wakatuletea kondomu. Mambo haya ni mageni kwetu. Kutoka kuzaliwa, uliona wapi kondomu wewe? Leo unaambiwa kuwa pia ni utaratibu wa maisha katika jamii. Tukakataa hivyo maana walituambia kwanza kuwa na mke mmoja. Sisi tumezoea wake zaidi ya watatu. Quran yatuambia wanne lakini wakaja na kusema kuwa kila mmoja awe na mke mmoja. Sasa jamani wanawake wote hawa duniani idadi ilikuwa ni kubwa kutoka enzi za Mfalme Herode. Wanawake walituzidi umri na idadi kwa sababu ulifika wakati wanaume waliuawa. Leo tunajaribu kuwapa nao hali za kuwa wapate kuwa na maboma. Limekuwa pia ni tatizo kwamba ni lazima hayo tuyaache. Tuliyakubali shingo upande ikawa hatuna budi. Nafikiria tumeendeshwa vibaya kwa muda mrefu na ni jukumu letu sisi wenyewe tujijue. Huku wanakotupeleka ni wapi? Ndiyo maana naomba kwamba wakati umefika tuanze kufanya maamuzi sisi wenyewe kwamba hili hatulitaki. Hii ni kwa sababu lilipoingia hili suala la mashoga na wasagaji wapate kutambuliwa, basi sijui mwanadamu alikuwa ameingia usingizi gani mpaka tukafika kiwango hicho lakini yote tukasema pia ni wakati na yataisha. Naomba tujaribu kurudi kwa vitabu vya Mwenyezi Mungu kutafuta pale ukweli ulipo ili tupate kujijua na kujua tunaelekea wapi katika haya yote tunayoyafanya. Tusije tukapotoka na kuleta Sodoma na Gomora kabla ya ulimwengu kumalizika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}