GET /api/v0.1/hansard/entries/1223028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223028,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223028/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Katiba yetu imekataa mambo haya. Hata hivyo, angalia vile binadamu wanavyotumia njia za mkato na kuhakikisha kwamba yote haya si vitu tunavyoweza kufanyia mabadiliko kinyume na inavyotakikana kisheria. Ni wakati wa kuambiana ukweli. Wakati tunapojadili suala kama hili, tukumbuke kombo tunayoenda sisi. Hakuna malaika aliyetoka mbinguni kuja kutuambia kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha tufanye haya lakini tunayafanya na tunajua kwamba tunamkosea Mungu. Ninalaani vikali jambo hili. Hata kama halijafika kiwango cha kuwa sheria katika nchi hii, sisi viongozi tulilaani. La muhimu na la msingi, kwa mfano, unaporudi nyumbani, mtoto wako wa kiume akuambie tarehe 30 Machi ataolewa na mume mwenzake kisha iwe utawaalika Wabunge wenzako kwa harusi hiyo ya mtoto wako wa kiume atakayeolewa na mwanamume mwenzake, utasikiaje? Utawaambia nini Wabunge? Najua muda umekwenda lakini mambo kama haya tukienda kule nje, tutaendelea kuyapigia kelele na kuyazungumzia ili tuepukane na huu uchafu."
}