GET /api/v0.1/hansard/entries/1223032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223032,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223032/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Seme, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Dkt) James Nyikal",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Huu si mtihani wa Kiswahili; ni kutoa maoni yetu tunavyofikiria kuhusu mambo makubwa tuliyonayo hapa Kenya. Wachana na Kiswahili sanifu. Sikiliza ninayosema ni nini. Hilo ndilo la muhimu. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu tendo hili ni kinyume cha maumbile, utamaduni na Katiba yetu. Nikianza na maumbile, lengo la uhusiano kati ya mke na mume ni kuzaa. Hakuna lingine, iwe ni kwa wanadamu au kwa wanyama. Haya mambo mengine ya raha na mapenzi ni sisi tumeyaleta ingawa huo ndio mpango wa Mungu na hufanya kazi anavyotaka. Lengo ni kupata watoto. Tukiendelea kufanya mambo haya ya mke na mke au mume na mume kuhusiana itachukua muda gani dunia iwe bila watu? Tutabaki na wanyama peke yake kwa sababu wanyama hawafanyi matendo haya hata kidogo."
}