GET /api/v0.1/hansard/entries/1223037/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223037,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223037/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Seme, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Dkt) James Nyikal",
"speaker": null,
"content": "Sasa, tumeleta maneno mengi. Hata wanyama hawajaleta hayo. Tufuate vile ambavyo Mungu alituumba. Kazi ya moyo wa mwanadamu ni kupiga damu izunguke mwili wote. Huwezi kuibadilisha ifanye kazi nyingine. Madaktari husoma mwili ulivyoumbwa. Hawatengenezi mwili bali wanasoma tu jinsi Mungu alivyouumba. Wakileta mambo yao mengine, wagonjwa wao watakufa. Kuhusu uzazi, tunaleta mambo mapya eti ni mapenzi. Mapenzi ni kati ya mume na mke kuvutiana wawe pamoja na wazae mtoto. Hakuna jambo lingine. Ndani ya mke kuna mfuko wa uzazi. Ikiwa Mungu angetaka wanaume wazae angewapa mfuko wa uzazi. Huo mfuko ndani hukuza mtoto hadi wakati atakapokuwa tayari kuishi duniani na kutoka kupitia njia aliyotengeneza Mungu. Sasa njia hiyo itafanya nini ikiwa mke na mke wameoana? Tusifikirie kuwa kama binadamu tumesoma; tunasoma tu jinsi ambavyo Mungu aliumba dunia. Tukitumia njia nyingine tutaharibu dunia. Utamaduni wetu unatukataza tabia hii. Hata ugenini, watu wengi wanaoana mke na mume; ni wachache tu ambao wana tabia hii na wanaleta kelele nyingi duniani ilhali ni wachache. Tuendelee vile Mungu alivyotuumba. Mimi ni mtu wa sayansi na pia ninaamini Mungu. Ukisoma Bibilia, Agano la Kale, Genesis 26, 27 na 28, utaona kuwa Mungu aliumba dunia, akaumba viumbe vingine na mwisho akamwumba mwanadamu na akamwambia viumbe vyote ameviweka chini ya ulinzi wake avilinde na kuvitumia. Ukitaka kuvitumia hivyo viumbe, lazima ufanye utafiti ili ujue Mungu aliviumba namna gani. Tukitaka kutibu watu, lazima tufanye utafiti na tusome mwili wa binadamu ulivyoumbwa na Mungu ndiyo tuwatibu. Hata ukiangalia vifaa ambavyo tunatumia kama ndege, watu wanaviunda baada ya kusoma na kuzingatia vile ambavyo Mungu aliiumba dunia. Tunaiga mfano wake. Unafikiri kuwa ni mhandisi ndiye aliamua kuwa chuma ni kigumu kuliko mbao? Hivyo ndivyo Mungu aliviumba vitu hivyo. Mhandisi huamua tu kuwa ukitaka kujenga nyumba kubwa, unatumia chuma. Ikiwa ni nyumba ndogo, unatumia mbao. Hata ukizingatia madini tunayoyatumia, ukijumuisha yale yanayotumiwa katika vita vya nyuklia kama uranium na titanium, sio sisi ambao tumeyaumba. Sisi tunasoma tu na kufanya utafiti kuhusu vile ambavyo yameumbwa na Mungu. Hakuna tofauti kati ya sayansi na dini; ni kitu kimoja tu. Hata tukizingatia mambo ya genes na DNA, mtu wa kwanza kuyagundua alikuwa askofu, na hakuenda shule. Aliangalia maua na kusema kuwa kuna kitu ndani yake kinachoitwa “gene”."
}