GET /api/v0.1/hansard/entries/1223041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223041,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223041/?format=api",
    "text_counter": 140,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi Kaskazini, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Owen Baya",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Hoja hii iliyoletwa na ndugu yetu, Mbunge wa Nyali, Mohamed Ali. Moja kwa moja, naunga mkono Hoja hii iliyowasilishwa kuhusu Wakenya kupiga marufuku mahusiano ya jinsia moja. Mahusiano ya jinsia moja ni hatia kikatiba, na ni hatia kwa Mwenyezi Mungu kama vile Mohamed Ali alituonyesha katika Koran na Biblia. Mambo haya mageni ambayo yameingia nchini na kujaribu kukithiri katika taifa la Kenya yamesababisha vifo vya vijana wetu. Kuna vijana hapa Kenya ambao wamefariki ama wameuawa kwa sababu ya maneno haya. Yanahatarisha maisha ya vijana wetu. Kama kiongozi na Mbunge wa Kilifi, nasema kuwa lazima tuyaharamishe haya maneno. Kuna jambo moja katika Hoja hii ambalo lazima tuliangalie. Jamhuri ya Kenya inaongozwa na Katiba. Ukiangalia maandishi ya Mbunge ambaye amechapisha Hoja hii, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}