GET /api/v0.1/hansard/entries/1223046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223046,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223046/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi Kaskazini, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "Ama unasemaje gwiji wa lugha? Hiyo si ni sawa? Uhuru wa fikra, uzungumzaji na kujieleza, uko katika Atikoli 33 ya Katiba yetu. Mhe. Spika wa Muda, pengine utupatie mwelekezo. Je, Hoja hii inayojaribu kukanyanganyana na Katiba yetu ya kitaifa inaruhusiwaje kuingia katika Bunge? Tunawezaje leo hii kupiga marufuku uzungumzaji? Kuzungumza ni haki ya kikatiba. Uchapishaji ni haki ya kikatiba. Usambazaji ni haki ya kikatiba. Ijapokuwa Katiba inasema kwamba hata tukifanya hivyo, lazima tuzingatie mambo mengine kama maadili ya kitaifa. Hiyo ni sawa kabisa. Lakini kuna haki ya kikatiba ya kuzungumza. Ni haki ya kikatiba. Huwezi leta Hoja ndani ya Bunge hili kukanganya uhuru wa kikatiba, ijapokuwa mahusiano ya jinsia moja yanaharamishwa katika Katiba. Naunga mkono Hoja hii moja kwa moja. Lakini Wakenya ambao wamesoma sheria kule nje wanajua kwamba tayari mahusiano ya jinsia moja yamepigwa marufuku ndani ya Katiba. Kwa hivyo, hata tukizingatia Hoja hii hapa Bungeni, hakuna jambo ambalo tunafanya tukisema kwamba tupige marufuku mahusiano ya jinsia moja kwa sababu Katiba ishayapiga marufuku."
}