GET /api/v0.1/hansard/entries/1223055/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223055,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223055/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi North, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, yale maneno ambayo Mhe. Tandaza amesema yameonyeshwa katika Katiba. Anasema kwamba huwezi ongea kuhusu mambo ya kukatana ama kupigana. Katiba imesema hivyo katika mabano ya pili katika Ibara ya 33. Mambo ya ushoga, usagaji na hayo mengine yote ni mabaya kwa taifa la Kenya. Lazima sisi sote tusimame na Katiba yetu. Katiba inasema kwamba imeharamisha maneno ya ndoa za jinsia moja. Kama Bunge, hatuwezi kutunga sheria nyingine kusema kwamba ati tunaharamisha ndoa za jinsia moja, kwa sababu Katiba ishaziharamisha. Lile ambalo lipo na tuliongee ni kwamba tumeanza kuona mtindo mpya katika mahakama zetu. Tumeanza kuona mtindo mpya wa kwamba haya maneno yanasambazwa. Tumeanza kuona mtindo mpya kwamba kuna vijana na watu wetu wanashiriki haya mambo, na tunayalaani. Lakini, kuleta Mswaada kusema tupige marufuku ni kufanya kazi mbili ambayo ni moja. Katiba ishapiga marufuku. Kazi yetu, tunapokaa kule kwenye mabaraza, ni tulaani haya maneno na vitendo ambavyo vinatendeka. Tukae kule na tuseme kwamba makanisa na misikiti izidi kuelimisha Wakenya kuhusu mambo ya Katiba. Wazidi kuelemisha watu kwamba ni marufuku watu wa jinsia moja kuoana. Tuhakikishe kwamba hii sheria inatekelezwa. Tuwaambie watekelezaji wa sheria hizi za Kenya - maaskari, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na mahakama - wahakikishe kwamba kwa mambo ambayo Katiba imesema sio halali, tuhakikishe kwamba inatekelezwa. Hilo ndilo jambo letu sisi kama viongozi. Lakini sio sawa sisi ambao tulipitisha hii Katiba kurudi hapa tena na kusema tufanye maneno ya mahusiano marufuku. Katiba ishasema hili. Sheria na Katiba yetu zishasema kwamba sisi, kama Bunge, hatuwezi kupiga marufuku uhuru wa kuzungumza."
}