GET /api/v0.1/hansard/entries/1223065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223065,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223065/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante sana Spika wa Muda. Ningefurahia kwamba Mhe. Mohamed Ali angetuletea vipengele vya Penal Code. Kisha, avibadilishe, aweke faini iliyo kubwa zaidi na kifungo kilicho kikubwa zaidi kwa wale ambao wanahusika na maneno haya, na tuweke mkazo. Kisha, kama vile Mhe. Gikaria amesema - ambalo haliko katika hii Hoja - lazima tubadilishe Penal Code na tusema kwamba watu ambao wanashiriki katika hizi ngono za jinsia moja wapigwe faini kubwa. Isitoshe, hata tuseme kama ile sheria haionyeshi wafungwe miaka mingapi, tuseme anayeshiriki ngono hii hata anyongwe kwa sababu anafanya haya maneno. Hiyo ndiyo itafaidi ile inaitwa kwa Kiingereza to give effect toan Article. Mhe. Spika wa Muda, utaniruhusu niseme hiyo. We need to give effect to the Article ambayo imeharamisha maneno ya ngono ya jinsia moja. Tukifanya hivyo, tutakuwa tunasongeza sheria za Kenya mbele, na zitakua ni sheria zinazotufaidi zaidi."
}