GET /api/v0.1/hansard/entries/1223067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223067,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223067/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitui Kusini, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Dkt) Rachael Nyamai",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili pia mimi nizungumzie jambo hili; Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Mohammed Ali. Ameeleza vizuri madhara ya ndoa za jinsia moja. Jambo hili linazungumziwa kila mahali. Naanza kwa kusema kwamba naunga mkono Hoja hii. Hili ni jambo ambalo linasikitisha sana. Jambo ambalo linazungumziwa sana leo - katika televisheni zetu, mitandao, shule, makanisa, ofisi za serikali, vijiji na miji - ni maneno ya ushoga na usagaji. Hata mdomo wangu uko na shida kusema “shoga”. Ni kama nimesikia hilo neno mara nyingi, lakini hili la usagaji linanisikitisha sana katika akili. Ninajaribu kulinganisha usagaji na wasagaji katika lugha yangu ambako nimetoka, lugha ya Kikamba, na jambo hili linanitatiza mimi. Tunaunga mkono kwamba jambo hili linafaa kuchukuliwa kwa makini sana. Kama viongozi, na mimi kama Mbunge wa Kitui Kusini, tunaona ni kama Wazungu wameamua kutumaliza. Tunapotembea huko kwao, tunaona kuwa idadi kubwa ya watu wao ni wazee sana. Watu wa rika dogo, kutoka mwaka mmoja hadi watu wa miaka arobaini na tano ambao ni wafanyikazi, ni wachache sana. Tunaona ni kama wanatuonea wivu. Ni kama wanataka sisi pia katika nchi za Kiafrika na Kiarabu tuwe hatuna watoto ambao watatuzalia wajukuu. Mhe. Spika wa Muda, najua pia wewe utataka kuwa na wajukuu siku moja. Hata mimi nitataka kuwa na wajukuu siku moja ili nione wanavyokaa na vile mtu husikia akiwa na wajukuu. Ni jambo la kusitikisha watoto wetu wakiamka kila asubuhi na kulala kila jioni kuambiwa vile ndoa za jinsia moja ni nzuri, na vile kuna pesa huko kwa Wazungu. Mhe. Spika wa Muda, niliangalia video ya kusikitisha sana leo. Ni video ya mwanamke anayeelezea kwamba yeye alikua na watoto watatu. Na baadaye, kupitia maarifa ya daktari huko uzunguni, amegeuzwa na amekuwa mwanamme. Anasema, alipoanza kufanya jambo hili, hakuna mtu alimwambia kuna madhara mabaya sana ya kugeuka kuwa mwanaume. Anasema alipitia kupewa antibiotics raundi kumi na saba, na amefanya oparesheni saba. Lakini, alipokuwa anaanza, hakuna mtu alimwambia kwamba jambo hili ni ngumu. Sasa hii ana regret. Anajuta ni kwa nini alianza jambo hili. Wanapotuambia maneno ya ushoga na usagaji, hakuna mtu anatuambia ya kwamba utakua unajiuliza kwa nini ulianza kufanya jambo hili ukishaingia kufanya jambo hilo kwa miaka kumi. Kwa hivyo, nasikitika sana kwamba Mahakama ya Upeo – ambayo inafaa kukatiza mambo haya na kuyanyamazisha kabisa – ilipeana uamuzi ule. Umetuambia tuwe na tahadhari tunapozungumza ili tusizungumzie Mkono wa Serikali unaofanya kazi yake. Lakini, hili ni jambo linalofaa liangaliwe. Nashukuru Mhe. Kaluma sana kwa kuwa amelirudisha katika mahakama hiyo ili liangaliwe. Jambo hili halifanyiki katika miji mikubwa peke yake. Limeanza kuzungumziwa hata kule mashinani ambapo halikuwa linazungumziwa - sana sana, watu wakisikia kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}