GET /api/v0.1/hansard/entries/1223068/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223068,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223068/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui Kusini, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Dkt) Rachael Nyamai",
"speaker": null,
"content": "makanisa za Uzunguni na Marekani yameanza kuhalalisha mambo haya. Watu wanaanza kufikiria jambo hili linaweza kuwa namna gani kwa sababu pia dini inaizungumzia. Nafikiria kama Mkristo kwamba Mungu aliharibu Sodoma na Gomora alipoona inamsumbua. Aliiharibu mapema sana, katika kitabu cha Mwanzo. Hata hakungojea aje kuharibu huku mwisho wa Biblia. Alianza mapema. Kwa hivyo ni sisi, viongozi wetu wa dini, kiserikali, na pia sisi katika Bunge, tujue kwamba jambo hili limekuja kuharibu nchi yetu. Tuliangalie kwa makini na tulikatae. Mhe. Spika wa Muda, nimejitolea kuokota vitabu. Kwa sasa, nimepata vitabu vitatu ambavyo ni vya kihadithi tu vinavyofaa kusomwa na watoto wadogo. Nina imani kwamba kuna vitabu vingi katika nchi yetu ya Kenya ambavyo vinaendeleza uozo huu. Nafahamu kwamba kuna vitabu vingi katika nchi yetu ya Kenya vinavyoendeleza mambo ya ndoa za jinsia moja ama vijana kugeuzwa kuwa wasichana. Siku hizi tumeanza kusikia vijana wakisema wanajiskia kama wao ni wasichana, lakini jambo la kushangaza ni kwamba ukiuliza huyu kijana ni nini kinachomfanya ajihisi kama msichana, hata yeye anachanganyikiwa. Hii inamaanisha kuwa hakuna mahali ambapo anahisi mwilini mwake kuwa yeye ni msichana, ilhali ni kwa sababu jambo hili limezungumziwa sana na limeenea na limekuwa ni kama hali ya maisha ya kawaida. Kwa hayo, ningependa kuunga mkono jambo hili na niseme kwamba Wabunge tusimame imara, na tuwe wa kuhesabiwa kwa kukataa mambo ya wanawake kuwa na uhusiano na wanawake; kwa sababu yamekatazwa katika Katiba yetu. Tunastahili kukataa jambo hili kuingizwa katika shule zetu za msingi na za upili kwa njia ambayo imefichika kupitia kusomesha watoto maneno ya health promotion . Kwa kweli, sio health promotion, ila inamaanisha kuzungumzia maneno ya usagaji na ushoga ikiwa imefichwa katika mafunzo ya elimu ya afya. Naunga mkono jambo hili kama Mbunge wa Kitui Kusini, na niambie wananchi wetu wajichagulie wenyewe na sisi tuweze kukataa uharibifu wa familia zetu. Tusiwe kama hao, kwa sababu wameshaharibu nchi zao. Hawana watoto wala kukuza vizazi vyao vizuri. Kwa hivyo, tusikubali kuwekwa katika mjadala huu wa mashoga na wasagaji."
}