GET /api/v0.1/hansard/entries/1223084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223084,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223084/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Luanda, DAP-K",
    "speaker_title": "Mhe. Dick Oyugi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii ambayo imekuwa ikijadiliwa. Kwanza, ningependa kumshukuru ndugu yangu ambaye ameleta Mswada huu kwa sababu mambo ya ushoga ni mambo ambayo ni ya aibu, na ya kusikitisha sana katika nchi yetu. Nchi ya Kenya na vilevile katika Afrika. Jambo la ushoga ni jambo geni, lakini tumeona kwamba limekuwa na nia ya kupotosha vijana wetu. Vijana wengi wamepotoshwa na mambo ya kigeni ambayo si ya kiafrika na hayaambatani na mila, desturi na dini zetu. Bw. Spika wa Muda, kitabu cha Mambo ya Walawi Fungu la 20 kimezungumzia mengi kuhusu uovu unaofanyika duniani. Moja ya mambo hayo ni kuhusu ushoga, ambao sasa umezungumziwa sana na unakithiri sana katika nchi yetu. Nasimama kupinga na kusema kwamba ushoga hauna nafasi katika nchi yetu. Ni vigumu kuona mwanaume akifanya ndoa na mwanaume mwenzake; au mwanamke kufanya ndoa na mwanamke mwenzake. Haya ni mambo ya kigeni kwetu, na hayaleti furaha. Mambo haya yanaleta aibu na huzuni katika Taifa letu. Sijui ni taswira ipi ambayo tunafunza na kuwapa vijana wetu tunaposema kwamba mahusiano ya jinsia moja yanaweza kuzungumziwa na kukubaliwa katika nchi hii yetu ya Kenya."
}