GET /api/v0.1/hansard/entries/1223086/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223086,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223086/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Luanda, DAP-K",
    "speaker_title": "Mhe. Dick Oyugi",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, hivi karibuni tumeona katika vyombo vya habari kuwa kuna vikundi vingi vya vijana ambao wanajihusisha na mambo haya. Pia tumeweza kuwapoteza wengi kutokana na vifo ambavyo havikutarajiwa. Mungu alipomuumba mwanadamu, aliumba mwanaume na mwanamke. Hakuona ni vyema mwanaume aweze kuwa na uhusiano na mwanaume mwenzake. Katika maandiko, kulikuwa na miji wa Sodoma na Gomorrah. Wakati uovu ulikithiri na kujaa katika miji ile, Mungu aliona ni vyema abomoe na kuangamiza miji ile kwa sababu ya ushoga. Mimi, kama kiongozi, siwezi kukubali nchi yetu iwekwe kati ya nchi ambazo zina ushoga na zinakubali maovu ambayo yalimfanya Mungu kuangamiza Sodoma and Gomorrah nyakati zile. Itakuwa ni aibu na jambo la kusikitisha kuona nchi yetu imekuwa kati ya zile zina practice ushoga."
}