GET /api/v0.1/hansard/entries/1223092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223092,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223092/?format=api",
"text_counter": 191,
"type": "speech",
"speaker_name": "Naivasha, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Jayne Kihara",
"speaker": null,
"content": "kweli, hawatupendi. Wazungu walitutawala miaka mingi sana. Walipoondoka, sisi tulifikiri kuwa hawatalipiza kisasi. Lakini sasa inaoneka hiki ni kisasi. Kila tarehe 12 Desemba, sisi husherehekea jinsi tulivyo wafukuza wazungu. Inaoneka sasa wamekuja na ukoloni mamboleo ili watumalize sisi na watoto wetu. Walipoenda, hawakuacha kama watu wamesoma Afrika. Lakini sasa watu wamesoma na wamezaana na kuwa wengi. Hiki ndio kisasi wanalipiza kwa sababu sasa hawawezi rudi vile walikuja. Bw. Spika wa Muda, jambo hili halina utu na ni la kinyama. Sisi kama wazazi ambao tunataka wajukuu tukiambia waume waoe waume na wake waoane, hiyo ni kumaaanisha kuwa kuzaa kumekwisha. Vile tumeambiwa, Mungu aliweka kila tundu kwa kazi yake. Sasa inaonekana kuwa tutaanza kufunza watoto shuleni kazi ya kila tundu, kwa sababu sasa wameletewa mambo ambayo hayaeleweki. Tuwaambie watoto wetu wa kiume kuwa: “Tundu la nyuma ni la kuenda haja kubwa na kunyamba; sio la kufanya jambo lingine na mtu yeyeto. Na mtu akiwaambia hivyo, piga ripoti kwa sababu unaanza kufundishwa vibaya.” Siku hizi kama wazazi, tukisikia kuna harusi ya mvulana na msichana, tunafurahia sana. Hao wanasema waume waoane kwa waume, sijui wanataka wasichana watoe mabwana wapi. Jambo hili lazima lizungumziwe. Nashukuru Mhe. Ali kwa kuleta Hoja hii. Kusema kweli, tulikuwa tunaona haya kuzungumzia mambo haya. Mtu aliona haya kutamka tu neno ushoga. Kwa mfano, nimesikia neno usagaji leo. Sikulifahamu. Kwa Kiingereza ni lesbianism, na sikujua neno sawia la Kiswahili. Pia, tunajifunza Kiswahili hapa. Kama Wazungu wanataka kutusaidia au kutupa pesa za maendeleo, njia ya kufanya hivyo sio hii. Sio lazima tukubali mambo ya ndoa kati ya watu wa jinsia moja. Familia zitaisha. Watu wataisha na dunia itaanguka. Haya ni mambo ambayo yameangaziwa katika Bibilia. Leo hii tumeambiwa pia yapo katika Qur’an. Makanisa yameyazungumzia; Imams wametoa maoni yao. Katiba yetu imejieleza na sisi ndio tuliipitisha tukijua kuwa familia ndio mwanzo wa jamii. Kwa hivyo, kama tunataka kulinda jamii na watoto wetu, lazima tuunge Hoja hii mkono iliyoletwa na Mhe. Ali wa Nyali. Nilikuwa naona haya sana. Sikuwa nazungumzia mambo haya kwa sababu nilifikiri ni"
}