GET /api/v0.1/hansard/entries/1223094/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223094,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223094/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Naivasha, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Jayne Kihara",
"speaker": null,
"content": ". Lakini sasa tumeelezwa kuwa hii ni biashara ya pesa nyingi. Watu ambao wanashiriki katika mambo haya sio wakulima wadogo, bali ni watu walio na pesa. Kwa hivyo, jambo hili linaweza kuwavutia watoto wetu kwa sababu ya pesa. Tushikane na Uganda kupinga mambo haya. Pia tuambie watoto kuwa jamii huanza ambapo mke anaolewa na mume na wanapata watoto. Hivyo ndivyo Mungu alikusudia. Mungu aliumba mwanadamu na akili. Nafikiria mwanadamu ndio kiumbe aliyeumbwa na akili. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu na akili, mwanadamu anaelewa kuwa anaweza kuwa tu na mahusiano na jinsia tofauti naye. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunawezaje kushindwa na wanyama? Hauwezi kuona umbwa wa kike akiwa na mahusiano na mbwa wa kike, ama wa kiume akiwa na mahusiano na wa kiume. Kwa hivyo, tusiwe zaidi ya wanyama. Tunastahili tufundishe watoto. Hii dunia ina mambo. Lazima na sisi tumewekwa wakati huu ndio tuzungumzie hili jambo. Tunastahili tuambie watu, watoto wetu na kila mtu ya kwamba haya ni mambo mabaya sana. Naunga mkono Hoja hii. Ahsante sana."
}