GET /api/v0.1/hansard/entries/1223097/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223097,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223097/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Masinga, Independent",
    "speaker_title": "Mhe. Joshua Mwalyo",
    "speaker": null,
    "content": "na tujiulize Mungu alikusudia nini, na alisemaje? Kwa sababu mambo haya ya usagaji na ushoga ni ya nini? Kwanza ni kitu gani unasaga? Kwa maana kitu husagwa na kingine. Unasaga na nini? Haya ni mambo ambayo ni ya kigeni na hatuyaelewi. Ata Kiswahili chenyewe nafikiri kimetafutwa kijuu juu, kwa sababu mambo hayo hawakuweko. Hili ni jambo ambalo wale ambao wameyazungumza maneno hayo hawajui, kwa sababu imechukuliwa kijuu juu na haijulikani mwanzo wake. Kwa sababu pale mwanzo kwa Kitabu cha Mwanzo1:26, Mungu akasema na tumuumbe mtu na mfano wetu. Mstari wa 27 unasema na Mungu akaumba mtu kwa mfano wake. Kwa mfano wa Mungu aliumbwa mme na mke. Hawa waliumbwa wakiwa watu wa jinsia tofauti. Na hapo chini katika Mstari wa 28, inasema na Mungu akawabariki. Kubarikiwa ni kuambiwa endelea vizuri. Kama vile baba hubariki mtoto wake, anazungumza maneno mazuri. Anasema wewe utabarikiwa na utakua na mbuzi wengi. Utakua na kondoo na mali nyingi na hata shamba umebarikiwa. Umebarikiwa mjini na umebarikiwa nyumbani. Kwa hivyo, akawabariki na akawaambia hivi: “Zaeni mkaongezee na mkajaze nchi.” Mke na mme. Hawa ndio walibarikiwa na Mungu kwa kuzaa. Hatuoni mahali popote ambapo watu wa jinsia moja walibarikiwa na Mungu. Ni mke na mme waliobarikiwa. Ninamaanisha kuwa ile tofauti ya kubarikiwa ni kulaaniwa. Kwa hivyo, sasa hao wengine wanaojaribu kuiga kua wanawake na wao ni wanaume wamelaaniwa. Hivyo ndivyo ninavyomaanisha. Kwa hivyo, haiwezekani katika nchi yetu tuwe na watu ambao wanasema wanaoana na sisi kama wale tunaamini juu ya Biblia tunasema kwamba jambo hili linastahili kukataliwa kabisa na kuwekewa adhabu kali kabisa dhidi yao. Vile Biblia ilikua inasema katika Leviticus, kwamba watu kama hao wakipatikana wauawe. Kwa hivyo, sasa inatakikana adhabu kama hiyo iwekwe katika sheria zetu. Watu kama hao wakishikwa – yaani msichana kwa msichana ambaye wanadanganya wale wengine - wamalizwe ndio jambo hilo lisiendelee. Nunga Hoja hii mkono kabisa ili nchi yetu na Bara la Afrika lisipotoshwe na watu ambao wanaleta mambo ya kigeni. Kila mara tulikua tunaona mzee akioa bibi. Hawakua wakioa wanaume, bali walioa wanawake. Kwa hivyo, jambo hili tunalikataa kabisa kama Bunge. Tumesema hatuwezi kukubali mambo kama hayo kuingia katika nchi yetu. Kwa hivyo, tunawaambia watoto wetu wajihadhari na watu ambao wanawanong’onezea wakiwazungumzia mambo hayo ya kishetani. Sisi kama wazazi, Wabunge, viongozi wa nchi hii, tunataka tuwe na nidhamu; na pia watoto wetu mashuleni wapewe nidhamu inayofaa ili waendelee kubarikiwa, kuzaa na kuongezea nchi hii. Watu wakisema twende kwa njia hiyo, hata kura tutatoa wapi? Hakutakua na watu wa kutupigia kura. Watu wataisha! Wazee tulioko tukipita na tukiisha, watoto wetu watakua hawako kwa sababu watakua hawaongezei kama vile Biblia imebariki mke na mume kujaza nchi. Kwa hivyo, mimi naunga Hoja hii mkono ili tuendelee kuijadili, tuweke hiyo sheria na adhabu kali. Mimi namalizia hapo nikisema naunga Hoja hii mkono kabisa, na tuendelee. Mungu atubariki pamoja."
}