GET /api/v0.1/hansard/entries/1223109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223109,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223109/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Siku moja nikiwa katika safari zangu nikiwa rubani, tuliingia katika hoteli fulani ambayo sitaki kutaja jina. Tukipumzika hapo ndio tuendelee na safari katika mbuga za wanyama, nilifika nikaona akina mama wengi. Sasa ikawa mwanaume ni mmoja ambaye ni nahodha wangu. Nilikuwa mdogo wake. Kuuliza hapo, tuliambiwa walikuwa wanaume na wanawake ambao wameoana. Wamechoka na stress za wanaume. Yaani, tunaelekea wapi sisi? Usagaji na ushoga ni njia kubwa ya kusambaza maradhi. Tunajua hivyo. Sasa tunataka nini sisi? Jambo hili linachangia sana katika kuvunjika ndoa. Ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya mambo kama haya. Sasa ukimpata mwanamke anafanya mambo haya au atumie hizo vifaa wanazotumia, mwanaume akienda anamuona hayuko kamili, si ndoa itavunjika? Vile ndugu yetu, Mhe. Mohamed Ali amesema, wasichana wanauliza kama wanaume watawaweza. Utaniweza na wewe hutumii ile Mungu aliumba bali unatumia vitu vingine? Mambo haya yanavunja ndoa. Wanawake au wanaume hawataki kuoa wala kuolewa kumbe mambo ni hayo. Sio kwamba hawajapata wachumba. Naunga mkono kupinga marufuku kabisa usambazaji hizo vitabu na jambo lolote ambalo litaendeleza kutoa habari za usagaji au ushoga. Haya mambo yasikitisha. Mwenyezi Mungu ametuumba na ametengeneza njia za kufaa za kutumika lakini sisi twataka kutumia zingine. Wanadamu sijui tuko vipi. Mwenyezi Mungu ametuonyesha njia ya kufaa ambayo inaleta watoto. Lakini yeye lazima aende akaonje njia zingine ambazo hazifai. Na kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}