GET /api/v0.1/hansard/entries/1223110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223110,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223110/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "alivyosema Mbunge mwenzangu, ukionja leo, basi inakuwa kama ni mdudu sasa utabidi uonje siku zote. Wanawake ni wengi duniani na ni maumbile ya Mwenyezi Mungu. Alituumba na akapanga hivyo. Sasa, tukiwa tuko wengi na wanaume waende wakafanye ushoga, kweli hawa wanawake wataolewa na nani? Tunaomba ndugu zangu hapa, Wabunge wenzangu, tafadhali, tufanye lolote... Nimeshangazwa na Mbunge ambaye amesema hili jambo haliko kwa Katiba. Iko kwa Katiba sahihi. Hili jambo ni haramu na limekatazwa na Katiba kwa sababu haiwezi kuchangia zaidi kwa sababu ya pesa. Wacha zikae kwa sababu sio kila kitu. Tunataka utulivu wa roho na rehema za Mwenyezi Mungu. Tunataka Mwenyezi Mungu atubariki. Tukiangalia, kama vile ilivyokuwa nyuma, mazao yalikuwa mengi. Ikifika mwezi wa nane, Kenya kulikuwa na utajiri mwingi, lakini saa hii unapanda na unatafuta mbolea. Hata hakukuwa na mambo ya mbolea zamani. Haya mambo yote ni laana zile tunazopewa. Hawa mashoga na wasagaji wanalaana ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ukiwaona wenyewe ni watu ambao wanaweza fanya lolote. Hawajali. Ile tabia imebadilika na hawana haya. Mhe. Spika wa Muda, nataka kukomea hapa. Naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Mohamed Ali. Asante."
}