GET /api/v0.1/hansard/entries/1223121/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223121,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223121/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": "Haina haja sisi kama Wakenya tuanze kuzungumzia, kuchapisha na kujadialiana kuhusu swala ambalo mila, tamaduni na Katiba yetu inakataa. Maswala ya usagaji na ushoga ambayo kwa lugha ya kimombo isiwe mjadala wala mazungumzo kwa watu wa Kenya. Tunasema, it is a no-go-zone . Kenya inafahamika kama taifa linaloenzi Mwenyezi Mungu. Kuna dini tofauti lakini juu ya tofauti zetu za kidini, nashukuru ya kwamba sote tunazungumzia jambo moja. Tunalikataa swala la usagaji na ushoga kulingana na mila, desturi, tamaduni na dini zetu. Kama vile mzungumzaji mmoja alivyozungumza hapa, sisi tunaamini Mwenyezi Mungu na tunasema ya kwamba kazi ya Mungu haina makosa. Mwenyezi Mungu wakati wa kutuumba, aliumba Adamu na Hawa. Hii ni kumaanisha ya kwamba kuna mwanamke na mwanamume. Viumbe vyote mbali na binadamu, ambavyo Mwenyezi Mungu ameviumba, ameviumba vikiwa viwili viwili. Hii ni kumaanisha ya kwamba mwanamke anapaswa kuwa na mwanamume, na mwanamume better-half wake huwa ni mwanamke. Mimi nataka niseme hivi, kuna mwimbaji mmoja kule Tanzania anayeitwa Mwanahawa Ally, na kuna nyimbo ameimba akisema, “Umaskini wangu haunipi tahayuri.” Isiwe watu wanakuja kutugandamiza hapa ili tuweze kukubali Hoja hii kwa sababu ya umaskini wetu. Sisi hatutauza utu wetu kwa sababu ya pesa. Tutasimama gangari na kuhakikisha kuwa haya maneno hayawezi kutuathiri na watoto wetu ili tuendelee na maisha yetu vile tumekuwa tukiishi. Hao watu ambao wanajaribu kusukuma Hoja hii wananishangaza sana. Kwa nini wanalenga Kenya kiasi hii? Wametamani makalio ya wanaume wetu hapa Kenya. Wamejaribu kila mbinu. Hivi sasa, wanajaribu kuleta vitu havieleweki. Kama mwanamke Mkenya, nataka niwaambie wanaume wetu ya kwamba sisi tunawapenda na msishike mkondo huo, ili kuhakikisha ya kwamba mambo yetu yamekuwa sawasawa. Kuna ule Mjadala ama uamuzi ambao ulipitishwa na Mahakama Kuu. Tangu hilo jambo ama huo uamuzi wa Mahakama kuu utolewe, nimekosa usingizi mpaka dakika hii. Hii ni kwa sababu hali ya uchumi wetu kwa saa ni ngumu. Tukiruhusu mjadala ama hao watu waungane kwa makundi tofauti tofauti, kuna vijana ambao hawana kazi kwa dakika hii na wale maisha yao kwa sasa ni magumu kwa sababu shetani yuko na nguvu na safari hii, amekuja na pesa. Vijana wetu na watoto wetu watadanganyika na pesa na kujiweka katika vikundi hivyo vya usagaji na mashoga na ndipo ambapo tutapoteza watu wetu."
}