GET /api/v0.1/hansard/entries/1223159/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223159,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223159/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu East, KANU",
"speaker_title": "Hon. Jackson Lekumontare",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Hoja hii. Namshukuru ndugu yangu, Mbunge wa Nyali, kwa kuileta Bungeni. Sisi kama wananchi wa Kenya, tunaongozwa na desturi na mila zetu za kiafrika, na ata dini zetu. Kitabu takatifu cha Mungu, Bibilia, inasema ya kwamba mwanamke atawaacha wazazi wake, na mwanaume awaache wazazi wake, na wataungana kuwa kitu kimoja. Sisi Wakenya tunaongozwa na neno la Mungu. Kwa wale wasioamini dini, kuna mila za Afrika ambazo zinatuongoza. Kama viongozi, ni vizuri tusimame na kupinga yale tunayoletewa na nchi za nje kwa maana wale watu ambao wanaingia kwa nchi yetu ndio wanaotuletea haya mambo. Wanakuja kwa njia ya kutusaidia lakini ni vizuri ijulikane hasa wanakuja kwa sababu gani. Hii ni kwa sababu Kenya inategemea Mungu. Sisi hatutegemei msaada kutoka nje, maana Mungu mwenyewe anajua vile wananchi wa Kenya wataishi."
}