HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223165,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223165/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuria East, UDA",
"speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nashukuru kwa nafasi hii. Naiunga mkono Hoja hii ya Mhe. Ali. Kwanza, jambo mbaya linaonekana kwa jinsi linavyoletwa kwa umma. Katika dini zote, hakuna mahali popote ambapo jambo hili linawekwa wazi kwa maandishi. Ni jambo ambalo linaletwa kwa njia ya mkato na ya kinyuma nyuma. Ni jambo la giza. Ndio maana wanaolisukuma wanafanya hivyo kwa kutumia mifumo mingine tofauti na dini yoyote inayojulikana. Pili, katika tamaduni zetu, ni vigumu sana kupata tamaduni yoyote inayo kumbukumbu ama ata mazungumzo yaliyonakiliwa yakitaja mambo haya. Nitokapo katika jamii ya Wakuria, hata jambo la kutaja zoezi hili au uchafu huu haupo. Hatuna neno ambalo linazungumzia machafu haya. Yanakuja kutafutiwa majina kutoka maeneo mengine, na hata haya majina ukiyatafuta utakuta kwamba ni ya kuunganishwa ili yaweze kutia maana fulani. Vile vile, ukitaka kujua kuna tatizo hapa, inakuwaje kwamba jambo hili lazima lisukumwe kwa masharti? Eti, “ili niwape pesa, lazima mvumilie watu wa aina hii. Ili tuwafanyie hivi, lazima mvumilie watu wa aina hii.” Yaani masharti yaliyowekwa katika jambo hili ni masharti ambayo yamekuja katika namna fiche. Hili jambo halifai katika utamaduni, uchumi wetu na maandhari yeyote utakayoweza kufikiria bali, linasukumwa tu na nchi za kigeni kwa minajili ya kuwafurahisha watu fulani. Kama ni nzuri, mbona lisibaki kwao? Wanatutangazia na kutusambazia ili tufanyie nini? Ikiwa wanaona likiwa nzuri, wangebaki nalo. Hii ni kwa sababu kama kitu ni nzuri, utatamani kiwe chako. Kwa hivyo, ninalipinga hili jambo sana. Tusiruhusu kamwe. Tusiruhusu Mahakama yetu ya Upeo wapatiane ruhusa. Lazima tusungumze na wao. Wanakubali aje mambo kama hayo ilhali mnajua vizuri kuwa hii nchi inawaangalia na kuwaamini muweze kutoa mfano mzuri kwa ajili ya watoto wetu na kizazi kinachokuja? Mhe. Spika wa Muda, baadhi ya waliotoa hukumu hii ni wa jinsia tofauti, ya kiume na kike. Wengine wao wamepata kazi hiyo kwa sababu ya jinsia yao. Umepata kazi kwa sababu jinsia yako ni ya kike na leo hii, unatamani akina mama wasikuwepo? Hivi ndivyo tutatafsiri, ya kwamba unataka akina mama wasikuwepo kwa sababu umehitimu na umepata cheo cha juu Zaidi, ndio maana unataka mama aoe mama mwenzake. Itakuwaje? Tukikufungia kwenye chumba na mama mwenzako, mtazaa mtoto? Ni nani unataka azae watoto kisha wewe ukuje uwapapase papase na kuwageuza? Mhe. Spika wa Muda, inahitaji mtu apewe hukumu ya kifo. Haiwezekani kamwe kuwa wanaume wangoje mwanaume na mwanamke wazae watoto, watuletee kizazi kizuri baadaye, mwanaume anaenda kufanya mambo ya kipumbavu na mwanaume mwingine. Kesho itakuwa aje? Kwanza wewe kiongozi ambaye unatutangazia haya umesoma katika shule zetu na kupitia tamaduni zetu, kisha unataka mwanaume afanye mambo ya kipumbavu na mwanaume mwenzake ili kizazi kife, itakuwa aje? Unataka ubaki peke yako? Utafanyia nini hii dunia peke yako? Ikiwa Mungu mwenyewe alisema hakuijaza dunia ndio maana akatutuma sisi kuijaza, wewe unayetaka kizazi kisimame, unataka kuifanyia nini dunia hii? Ikiwa wanaume watabaki bila kupata watoto kwa sababu hawana uwezo wa kuzaa, mwanamke akimtamani mwanamke mwenzake, na mwishowe wasizae, ina maanisha dunia itabaki bure. Itakufaidi nini? Ya mwisho ni kuwa yale mashirika yasio ya serikali (NGOs) yametuletea matatizo mengi sana. Katiba tulio nayo na iliyotengeneza Mahakama ya Upeo, imekuwa na msukumo wa yale mashirika yasiyo kuwa ya serikali. Walipopata faida, walikimbilia hizi kazi kubwa. Tukiwachunguza, sio ajabu kuwa katika historia yao walikuwa katika NGOs yaliyokuwa yakisukuma mambo ya kipumbavu na ya giza kama haya. Nikimalizia, hili jambo sio la kusema tufanye hivi ama vile. Kila Mkenya anapaswa kukataa. Haiwezekani turuhusu watu kuzungumzia, kutangaza au kufanya jambo lolote linaloendeleza giza ya aina hii. Ninataka kuachia hapo lakini niseme kuwa kama Wakuria, hatutaruhusu mambo kama haya. Hii ndio maana kwenye Kaunti ya Wakuria, hili jambo halitaweza kukubalika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}