GET /api/v0.1/hansard/entries/1223170/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223170,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223170/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Turkana County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Cecilia A. Ngitit",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Bw. Spika wa Muda, ingawaje Kiswahili kinakanganya, nitajaribu sana ili mwalimu wangu wa Kiswahili, Bw. Joseph Kaikai Nabwimba, askie vizuri aliko. Ningependa kupeana kongole zangu kwa Mjumbe mwenzangu, Mhe. Mohamed Ali, kwa kuleta Hoja hii. Ningependa kupinga hili jambo la ndoa za jinsia moja kwa sababu jambo hili linaenda kinyume na neno la Mungu. Sisi Wakenya ni waumini wa neno la Mungu. Wakati Mungu aliumba dunia, aliumba binadamu na wakati aliona ana upweke, hakumuumbia mwanaume mwenzake, bali alimuumba Hawa ambaye ni jinsia tofauti. Hivyo inamaanisha Mwenyezi Mungu anataka ndoa za jinsia tofauti, yaani mume kwa mke sio mume kwa mume wala mke kwa mke."
}