GET /api/v0.1/hansard/entries/1223172/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223172,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223172/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Turkana County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Cecilia A. Ngitit",
"speaker": null,
"content": "inayounga mkono jambo hili. Hata Katiba yetu inaenda kinyume na hili neno. Katiba yetu inatambua ndoa za jinsia tofauti ambayo ni mume kwa mke. Kama vile wenzangu walivyosema, mila zetu ziko na sababu zao na matumizi. Kama vile wenzangu walivyosema, miili zetu iko na sababu zao na matumizi. Wenye wanashiriki jambo hilo la mume kwa mume wanaumia sana kiafya. Unashtukia unaposoma wamefanyiwa upasuaji kwa sababu ya kutumia sehemu za mwili kwa njia ambayo haifai. Haya mambo ya mashoga na wasagaji, wanasaga nini? Nilishangaa sana eti hawa watu wamechukua rangi ya upinde wa mvua. Rangi safi na nzuri sana. Ukiangalia mkono wangu nina bangili niliopewa na mpiga kura wangu kama zawadi ambayo iko na rangi iliyo na sura nzuri ya upinde wa mvua lakini nimeambiwa hiyo ndiyo alama ya hawa watu. Ukienda nyumbani kwetu sisi wafugaji, utapata tunapenda sana mambo ya shanga…"
}