GET /api/v0.1/hansard/entries/1223232/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223232,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223232/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Naomba niunge mkono ombi hili ambalo rafiki na jirani yangu ameleta katika Jumba hili ili watu wake waweze kwenda sokoni. Watu wake wanafunguliwa barabara siku mbili za wiki. Hili sio jambo la kawaida ya kwamba katika Kenya hii, kuna watu ambao ili waende mahali popote pale, lazima wangoje zile siku ambazo Shirika la Kenya Wildlife Services (KWS) limetenga ili wapitie barabara hiyo. Naunga mkono ya kwamba Bunge hili litatue jambo hili. Wakati Bunge linapoangalia barabara hii na zinginezo, pia kuna barabara ambayo inatoka Lolgorian inapitia Mara Rianta, Lemek kuja mpaka Ngorengore, ambayo iko na matatizo kama hayo. Tutakapoweza kuishughulikia, itakuwa ni barabara ambayo itafanya safari hiyo iwe fupi kutoka Nairobi, Muhuru Bay, Migori, Kuria hadi sehemu ya Lolgorian na Kilgoris. Safari hiyo itapunguzwa kwa kilomita 150. Lakini kwa sababu ya masharti mbali mbali ambayo yamewekwa, barabara hizi zimefungwa. Sisi tunapenda Wanyama. Wanaleta rasilimali katika nchi hii na ni maridadi. Lakini kuwa na wanyama isiwe ni kizingiti bali iwe ni faida kwa kila mtu. Mhe. Naibu Spika, naomba jambo hili liangaliwe kwa upana. Barabara hiyo aliyoisema Mheshimiwa na hiyo niliyotaja zishughulikiwe ili watu wa eneo hizo waweze kupata faida ya rasilimali ya nchi hii."
}