GET /api/v0.1/hansard/entries/1223252/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223252,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223252/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu wa Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Kusema kweli, hii kupimiwa kwa barabara, inaleta adhari nyingi sana. Sisi tunayapitia mambo haya Lamu. Imekuwa ni kama ya kawaida. Nimeshangaa kwa sababu nilifikiri ni Lamu peke yake ambayo inapata shida kama hizi. Ikifika saa kumi na mbili Lamu, barabara na Kaunti nzima inafungwa na hakuna ruhusa ya kutoka nje. Kukiwa na mambo ya dharura, ni gari la wagonjwa pekee ambalo linatoka. Katika sehemu zingine nilipatana na Special Force wakanisomea kama mtoto mdogo."
}