GET /api/v0.1/hansard/entries/1223454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223454/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa ili nipenyeze sauti yangu. Ningependa kuchukua nafasi kumpongeza Mwenyekiti wa Hazina ya Maeneo Bunge kwa kuleta majina ya maeneo Bunge matatu ili yaweze kupitishwa. Ni vizuri sana yapitishwe kwa sabau kuna shida kubwa sana mashinani. Watoto wengi hawaendi shule kwa sababu hawana karo. Shida zimekuwa nyingi. Kwa hivyo haya maeneo Bunge matatu ambayo majina yao hayajakuja yako katika shida kubwa sana. Naomba sisi sote tushirikiane kuhakikisha kwamba haya majina yamekuwa Gazzeted mapema sana kwa sababu hali ni nzito. Pia, ningependa nichukue fursa hii kumweleza mwenyekiti wa hazina hiyo kwamba ni muhimu aje hapa kutupatia taarifa kuhusu vipi fedha zitagawanywa, kwa sababu tangu kupeanwe fedha ni muda mrefu na mpaka sasa fedha hizo zingine hazijatoka. Imekuwa sasa mtu anatoa bursary ya F orm One, anangoja tena ndipo atoe ya F orm Two na kadhalika hadi"
}