GET /api/v0.1/hansard/entries/1223456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223456,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223456/?format=api",
    "text_counter": 276,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": ". Shida ni kubwa ndugu yangu mwenyekiti. Naomba uwasukume kwa sababu katika ahadi walizotoa tukiwa Pride Inn ni kwamba kila wiki mbili watatoa shilingi bilioni nne. Baada ya hapo hakuna kitu tumeona, hata ndururu! Hali ni ngumu sana. Watoto wa university hawaendi shule kwa sababu ya hali ngumu ya kimaisha. Pia nikutahabarishe Mwenyekiti kwamba Board ya NG-CDF ndiyo inaotoa maamuzi ni kitu gani kifanywe katika maeneo Bunge. Wananchi wamekuwa wakikusanyika wakitoa maamuzi. Kama eneo langu kuna uzoroto wa usalama. Sasa watu wanataka securitylights. Tumekubali tuweke security lights. Ikifikia hapo kwa bodi, wanasema haiwezekani ilhali watu wanaumia. Sio wao wako kule uwanjani. Hizi ni fedha ambazo wananchi wanajiamulia wanataka kufanyia nini. Wasikae hapa Nairobi kuamua. Kwa hivyo naomba uingilie kati hili suala, uwaambie kwamba wafuate taratibu zile wananchi wanataka. Kwa haya mengi nakushukuru Spika wa Muda. Ningependa nitoe nafasi kwa mwingine naye pia achangie. Asante."
}