GET /api/v0.1/hansard/entries/1223461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223461/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Embakasi South, WDM",
"speaker_title": "Hon. Julius Mawathe",
"speaker": null,
"content": " Nashukuru sana Naibu Spika wa Spika kwa kunipa fursa hii nichangie kidogo kwenye huu mjadala. Nataka kumshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya NG-CDF. Bwana Mwenyekiti, tungelitaka kama inawezekana tusukume National Treasury. Sharti tuhakikishe kwamba hizi senti za bursary zimepatikana. Kuna haja kwa sababu wazazi katika maeneo kama ya Mukuru kwa Njenga, Mukuru kwa Reuben na Riara ni watu wa mapato madogo. Hawana pesa za kuwapeleka watoto shuleni. Kwa hivyo, naomba kama inawezekana mzungumze na National Treasury tuwekewe pesa zote za NG-CDF na hasa pesa za bursary ndiposa tuweze kusomesha watoto wetu. Ni watoto wengi ambao hawakuweza kujiunga na kidato cha kwanza na mliwaona kwenye runinga. Wazazi wameshindwa kuwapeleka watoto shuleni. Kwa hivyo, tunaomba wewe, Kamati yako, na Bodi nzima mtilie uzito kidogo ndiposa watoto wetu waweze kupata bursary ndio waende shuleni. Kwa hayo mengi, nakupongeza kwa kazi uliyofanya na yenye unaendelea kufanya ili tuweze kupata hizi senti za NG-CDF. Asante."
}