GET /api/v0.1/hansard/entries/1223646/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223646,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223646/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante Bw. Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono mjadala wa wale ambao wamepata kazi ya mambo ya kupanda miti na mambo ya mazingira. Serikali iko na kibarua kikubwa sana kwa sababu tutapanda miti ambayo itatusaidia kutapata mvua na pia tutapata maji ya kukunywa. Ningependa kushukuru Serikali ya Kenya Kwanza kwa yale wamefanya. Tunajua wale watu ambao wamechaguliwa ni watu ambao wana elimu ya juu na ni watu ambao wanajua shida ambazo tuko nazo katika nchi ya Kenya. Wakifanya kazi nzuri kwa hiki kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Kenya Kwanza itapata nguvu ya kusema ile kazi ambayo imefanya. Kwa sababu hapo mbeleni, kama serikali zile zingine zingekuwa zinafanya kama serikali ya Kenya Kwanza inavyofanya, kama vile kufikiria mambo ya binadamu, sisi hatungekuwa vile tulivyo. Wiki iliyopita, tulikuwa huko kutathmini kama ndengu inawezakuwa cash crop . Endapo kaunti hiyo ama zingine kama Embu hazitazingatiwa, miti tutakayopanda haitakua vizuri. Kwa hivyo, tutakuwa tunafanya kazi ya bure. Tutakuwa tunatumia pesa za Serikali bila kupata mavuno mazuri."
}