GET /api/v0.1/hansard/entries/1223753/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223753,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223753/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, nilileta Statement wakati daraja hilo lilianguka ingawa hapo mbeleni, Mheshimiwa wa Eneo bunge la Siakago alikuwa amezungumza kuhusu hilo. Maafisa wa KeRRA walienda wakaangalia na kukarabati. Kulingana na maafisa wa KeRRA, kuna mambo tunayoweza kusema sisi kama Maseneta ambayo yanaweza kutuaibisha. Nilialikwa na kamati ya Seneti na tukaenda kuongea nao. Niliwaambia kuwa hakuna haja ya kufuatilia barua za KeRRA kwa sababu wakati mwingine maafisa wa KeRRA hufanya kazi vile wanavyotaka. Niliwaambia kuwa ili iwe funzo kwa maafisa wa KeRRA, waende pale na kuangalia jinsi daraja lilijengwa, kwa sababu miaka mingi ilikuwa imepita tangu lijengwe. Hata hivyo, mbeleni hatukuwa na magari mazito ya kupita pale na sasa yameongezeka. Niliwaomba waende waangalie ili kuona kama walifanya kazi jinsi ilivyofaa kwa sababu magari yanayopita pale si mazito kama ilivyokuwa awali. Niliwauliza kama walitaka niandike barua tena ili daraja hilo litengenezwe kulingana na uzito wa magari ya sasa."
}