GET /api/v0.1/hansard/entries/1223976/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1223976,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223976/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono taarifa iliyoletwa na Sen. Joe Nyutu wa kutoka Kaunti ya Murang’a. Mambo ya nguvu za umeme yamekumwa ni hali ya sintofahamu katika nchi yetu. Sio Murang’a peke yake. Ukitembea sehemu nyingi hasa katika Kaunti ya Laikipia unapata transformers ambazo tumepewa zinasambaza nguvu za umeme kwa mtu mmoja tu ilhali sehemu hiyo ina watu wengi ambao hawana stima. Mradi ule unaitwa Last Mile kwa lugha ya kiingereza. Hata hivyo, sisi watu wa Kaunti ya Laikipia hatuna tabasamu yoyote kwa sababu stima yenyewe hakuna. Tunaishi kwa giza. Taarifa hii isiangazie Kaunti ya Murang’a pekee yake. Waangazie hata Kaunti ya Laikipia. Hii ni kwa sababu baadhi ya transformers zinazoletwa ni gushi. Wakati huu kunanyesha, kukiwa na radi, unapata stima zinapotea na wakati mwingine bidhaa za nyumba zinaharibika."
}