GET /api/v0.1/hansard/entries/1223978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1223978,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223978/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Hivyo basi, Shirika la nguvu za umeme linapaswa liangazie haya mambo. Wanapoulizwa haya maswali, waseme ni transformer ngapi ambazo wamepeana huko Laikipia, watu wangapi wamepewa stima. Sio hayo tu, bei ya nguvu za umeme imepanda sana. Tumeambiwa kwamba hii ni kwa sababu hakunyeshi. Lakini pia kukinyesha mara moja tu, stima zinapotea. Unashindwa ni shida gani iliyoko. Wakati wa kiangazi, unaambiwa hakuna maji. Kukinyesha, unambiiwa maji yamekuwa mengi hivyo basi stima hatupati. Tungetaka tuambiwe ni watu wangapi wamepewa umeme kwetu Laikipia na ni watu wangapi wamepangiwa kupewa umeme wakati huu wanasema ni tabasamu na isiwe ni tabasamu ya mwisho. Hivyo basi, haya mambo yaangaziwe ndio yaweze kuongoza uchumi. Hii ni kwa sababu, wakati huu, uchumu umeharibika. Tukipata nguvu za umeme tunaweza kufanya kazi masaa ishirini na manne. Na nikitaja tu kwa sababu ndugu yangu alitaja na ni vizuri niseme, Seneta wa kutoka Homa Bay. Sen. M. Kajwang, alisema ya kwamba masomo si ya manufaa hapa katika Seneti. Sio vizuri akiwa anongea na wanafunzi wa chuo kikuu na kuwaambia---"
}