GET /api/v0.1/hansard/entries/1224456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1224456,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224456/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, kuanzia mwanzo, naunga mkono Hoja hii na marekebisho yote yaliyoko. Ni vizuri ijulikane kwamba tukisema Mawaziri watakuwa wakija hapa, haimaanishi hawatakuwa wakialikwa katika kamati zetu jinsi ilivyokuwa. Mambo mengine yananikera ninaposikia watu wakisema Bunge ni tofauti na uongozi mwingine. Huo ni ukweli. Hata hivyo, tumekuwa tukiwa na vikao vya Seneti nzima kama vile vya kamati kwa sababu huwa tunaalika Mawaziri hapa. Sen. Okiya Omtatah amesema kuwa Waziri hawezi kuja katika Seneti kwa sababu Mawaziri wanaalikwa na kamati. Bw. Spika, ningependa Sen. M. Kajwang’ anisikilize. Amesema kuwa watakuwa wanauliza Mawaziri maswali magumu ambayo watashindwa kujibu. Ningependa kumkumbusha Sen. M. Kajwang’ kwamba baadhi ya Mawaziri watakaokuja hapa ni kama Mhe. Kipchumba Murkomen na Mhe. Mithika Linturi ambao wana uzoefu. Tumekuwa tukisumbuliwa na maswali hapa. Kila wakati tukiuliza maswali, tunataka Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Sen. Joe Nyutu, ama Mwenyekiti wa Kamati ya Mashamba, Mazingira, na Rasilimali, Sen. Methu, wajibu. Hata hivyo, wanapoyajibu, tunasema kuwa hawajajibu jinsi tulivyotaka. Kwa hivyo, ni vyema Mawaziri waalikwe katika Seneti ili wajibu maswali magumu. Bw. Spika, nilikuwa hapa wakati tulimwalika Waziri Dkt. Matiang’i. Tulikuwa tunamuuliza maswali magumu na bado alikuwa akija. Kwa hivyo, tunafaa kuweka kwenye sheria ili wawe wakija hapa kuulizwa maswali na kujibu kwa sababu imekuwa kizungumkuti. Wakati Sen. Wambua anaongea mambo ya ndengu, ni vyema kumwita Mhe. Mithika Linturi ili atueleze kwa kina haya mambo. Tumekuwa tukizungumzia mambo ya usalama. Wakati operesheni inafanywa, tunauliza Seneta wa Baringo, ilhali ujumbe"
}