GET /api/v0.1/hansard/entries/1224693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1224693,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224693/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Spika wa Muda. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii kupinga kupiga marufuku uzungumzaji, uchapaji, usambazaji wa taarifa zinazohusiana na mapenzi ya jinsia moja. Sisi kama Waafrika tuna utamaduni wetu, desturi na mila zetu ambazo haziusiani na jinsia moja yaani wanaume waoane na wanaume na mwanawake aoane na mwanamke. Nchi hii ina sheria zake na kanuni zake ambazo ziko ndani ya Katiba. Mambo ya ushoga na usagaji yanaenda kinyume na mila na tamaduni zetu kama Waafrika. Tunapinga vikali kiini ama njia yoyote ambayo inaweza kuleta mauhusiano ya mwanaume kwa mwanaume. Hata shetani mwenyewe alipokua anamjaribu Hawa hakuenda kwa Adamu. Alijua ndoa ni ya mwanamke na mwanaume. Hii ni njia ambayo mataifa ya kigeni yanataka kutumia ili kuhakikisha ya kwamba ongezeko la wananchi katika bara la Afrika linapungua kwa kiwango kikubwa. Ni lazima kama Wakenya kupinga vikali na wale wote wanaotumika kueneza haya mambo ni lazima wachukuliwe hatia kali. Tunajua mbinu na njama, hii ni desturi ya watu wa nje kule America na katika nchi za Jumuiya ya Madola. Kama wanataka kufanya ushoga, wafanye kwao Ulaya na Amerika, watuwache sisi Waafrika tuendelee na mila zetu, dini zetu na desturi zetu. Hatuwezi kubali mambo ya ushoga na usagaji katika taifa letu. Asante Spika wa muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}