GET /api/v0.1/hansard/entries/1224695/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1224695,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224695/?format=api",
"text_counter": 79,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Spika wa Muda. Nami nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo ililetwa na Mhe. Mohmmed Ali ambayo kwa hakika tunasimama kidete kupinga maswala ya mambo ya ushoga. Taifa letu la Kenya ni taifa ambalo tuko na misingi ya kidini. Dini zote ndani la taifa la Kenya hazikubaliani na maswala ya mambo ya mashoga na usagaji. Mimi nataka niunge mkono nikisema kwamba napinga kikamilifu. Sisi kama Wakenya, ni watu ambao tunatii dini na kama nilivyotangulia kusema, dini hairuhusu maswali ya ushoga wala usagaji. Mimi nataka niunge mkono Hoja hii na Bunge hili la Kitaifa linapopitisha Hoja hii tuhakikishe kwamba sheria kali inatolewa kwa wale ambao watakua na matendo la ushoga ama usagaji. Asante sana Spika wa Muda nasimama kuunga Hoja hii nikilaani vikali sana maswala ya ushoga na usagaji katika Taifa letu la Kenya. Nataka kumshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Kenya kwa sababu amekua mstari wa mbele kupinga ile uamuzi ambao ulitolewa na mahakama. Uamuzi ambao ulikua unasema kwamba ushoga uweze kuendelea. Nataka nisimame hapa kumshukuru Rais wetu kwa kua kwa mstari wa mbele kupinga maswala ya ushoga ndani ya Kenya yetu. Asante sana Spika wa Muda, asante sana Mohammed Ali kwa kuja na Hoja hii."
}