GET /api/v0.1/hansard/entries/1224699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1224699,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224699/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": " Shukran sana Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuwasilisha Hoja hii na kwanza kabisa ningependa kuanza kwa kuwapongeza Wabunge wa taifa kwa kujitokeza na kuweza kuunga mkono Hoja hii wa kupinga matendo ya kishetani yanayojaribu kuletwa na wazungu katika taifa hili letu. Mimi nitaendelea kusimama kidete na kusema ya kwamba hatutakubali kamwe tabia za Wamerekani ziletwe hapa ili mashoga na wasagaji waweze kutawala nchi hii. Ningependa kumwambia Balozi wa Marekani humu nchini Bii. Meg Whitman kuwa ya kwao ayafanye Marekani na ya Kenya awaachie Wakenya. Mambo ya kutuletea mambo ya ushoga na usagaji na hata kutumia pesa kufikia viongozi mbalimbali na kutumia misaada haramu ili kuweza kuleta tabia hii mbovu humu nchini Kenya, hatutakubali. Kama wewe unajiona kama kiranja wa dunia ifahamike ya kwamba mkuu wa hii dunia ni Mwenyezi Mungu na katika dini ya Kikristo na dini ya Kiislamu na dini zingine zote, mwenyezi Mungu ameikataa. Ningependa pia kuchukua fursa hii niweze kumpongeza sana Rais Yoweri Kaguta Museveni. Mungu akupe afya na akuongezee umri kwa sababu jana ulitia sahihi ya kuhakikisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}